Habari

Habari kutoka Uholanzi

Oktoba 2009 - Tulianza ukarabati wa madarasa katika shule ya msingi ya Magutu. Mkurugenzi wa Mradi Rene de Vries alikuwa Kenya.

Julai / Agosti 2009 - pendekezo letu ni linaidhiniswa na NCDO.
Mkurugenzi wa Miradi Rene de Vries alikuwa nchini Kenya kwa wiki 6. Yeye na mkurugenzi wa nyanjani Rose Anami walitoa mafunzo ya tarakilishi kwa shule ya upili ya St Philip's Girls' Secondary School. ( Magharibi mwa Kenya). Walisimamia pia kisima cha maji safi ya kunywa cha shule ya Msingi ya Magale, Kambiri.)

Aprili 2009 Tutatuma pendekezo zingine mpya kwa NCDO

Februari 2009 Mwanachama wa FUSP Rene de Vries alikua nchini Kenya kwa wiki mbili na akafanya mkutano na wanachama wa shirika la kibinafsi la Bidii, wakajadiliana kuja kwa madakitari wa meno kutoka uholanzi, katika shule ya msingi ya Magutu na akapeleka tarakilishi katika shule.
Kazi ya madaktari wa meno katika shule ya Msingi ya Magutu ilikua ya fanaka sana. Bonyeza hapa kwa ukurasa mfupi wa picha.

Januari 2009 wanachama wa FUSP wa shirka la meno la  Dutch Dental Care Foundation (DDC). DDC iko tayari kuangalia meno ya wanafunzi wote wa Shule ya Msingi ya Magutu. Ikihitajika meno yatatibiwa. Wanafunzi, Waalimu na wazazi watapata maelezo mafupi na kupwa mswaki.Hii itafanyika februari 2009
Mwanachama wa FUSP Rene de Vries atakua Kenya pia kuhakikisha kuwa tarakilishi zilifika salama na pia kuziunganisha. 

Desemba 2008 usimamizi wa mashirika yasio ya kiserikali,nairobi inazidi kuchelewesha usajili wa shirika la Bidii, lakini tunaendelea kujaribu ili liweze kusajiliwa kabla ya mwisho wa mwaka wa wa 2008 (hata hivyo haitatushangaza Nairobi kikamilisha shughuli hii mwaka wa 2015.
Pia tuko na shida ya kupata tarakilishi. Tulikubalina kuzipata kutoka Bandari ya Mombasa ,kwa bahati mbaya ziko Malindi.
Kwa sasa hatuna fursa ya kuzichukua kutoka huko na kizipeleka katika shule zilizokatika miradi yetu..

Oktoba 2008 Mwanachama wa FUSP Rene de Vries alikua Kenya kwa wiki tatu (oktoba). Alifanya mkutano na wanachama wa shirika la Bidii, akatembelea shule na kuzindua ujenzi wa vyoo vipya katika shule ya Msingi ya Magale na kuekwa kwa bomba za maji zenye urefu wa kilomita nne za Shule ya Msingi ya Mwangea.
 

 
Kibali cha usajili na Ramani
Kwa wasio waholanzi ona  [ Michango ] ili kujua jinsi ya kutoa mchano wako.